
Victoria Institute Yaandika Historia yafanya Mahafali yake ya Kwanza
Chuo cha Victoria Institute leo, tarehe 25 Oktoba 2025, kimeweka rekodi mpya kwa kufanya mahafali yake ya kwanza tangu kuanzishwa kwake. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Iddrissa Abdul Wakil na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wazazi, walezi, pamoja na wadau mbalimbali wa elimu.
Katika sherehe hiyo ya kihistoria, wahitimu wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti vyao vya kitaaluma ikiwa ni ishara ya mafanikio ya safari yao ya elimu. Mkuu wa chuo aliipongeza juhudi na nidhamu ya wahitimu, akiwahimiza kutumia ujuzi walioupata kuchangia maendeleo ya jamii na taifa.